Welcome to Mwananyamala Regional Referral Hospital



Mwananyamala Regional Referral Hospital is a public facility serving the population of more than 2.2 million in Dar es Salaam and the surrounding areas, with Kinondoni and Ubungo districts as its definition area. Our Vision is to be a leading Regional Referral Hospital in the provision of Quality Health Services


Hospitali ya Mwananyamala yajipanga kwa vipimo vya kisasa

 Hospitali ya Mwananyamala yajipanga kwa vipimo vya kisasa, kuanza kupima MRI na CT Scan 2020


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu amesema ujenzi chumba cha vipimo vya mionzi (MRI na CT scan) unaendelea vizuri katika jengo jipya la ghorofa 4 linalojengwa kwa ajili ya huduma za mama na mtoto.

"Tunatarajia jengo la Mama na Mtoto litakamilika lote kufikia April, 2020. Lakini chumba cha CT Scan kitakamilika na kuanza kutumika mapema zaidi," amesema.

Dkt. Nkungu ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu wa hospitali ya Mwananyamala kupata kipimo hicho, hatua hiyo itawaondolea usumbufu wananchi wanaohitaji huduma hiyo na pia kuwawezesha wataalam kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Kwa sasa wagonjwa wanaohitaji huduma za MRI na CT Scan hupewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili au Mlonganzila.

Dkt. Nkungu ameishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli, kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ambao umewezesha kufanikisha ujenzi unaoendelea na ununuzi wa vipimo vya kisasa kama hivi vya MRI na CT Scan.