Mhe. Ummy Mwalimu akila kiapo Baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa TAMISEMI, 1 April 2021 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.
DODOMA. Aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
maziringa Mhe, Ummy Mwalimu amekula kiapo cha kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais,
Tawala za Miko ana serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kuteuliwa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Ummy ameapishwa katika Hafla iliyofanyika Tarehe 2
April 2021 Ikulu ya Chamwino Jijini Dododma ya kuwaapisha Mawaziri wa wizara Mbalimbali
walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Awali Wizara hiyo ya TAMISEMI ilikuwa ikisimamiwa na Mhe,
Suleiman Jaffo ambaye aliteuliwa na Hayati Magufuli akiwa Raisi na kudumu
kwenye Nafasi hiyo kwa kipindi cha Maika mitano ya awamu ya Tano.
Kabla ya Mhe. Ummy Mwalimu kushika Nyazfa hizo Mbili
Alikuwa Waziri wa Afya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Kipindi
cha Miaka Mitano ya Awamu ya Tano Baada ya kuteuliwa na Aliyekuwa Raisi wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika Kipindi alichokuwa waziri wa Afya Mhe Ummy
alisimamia Kikamilifu Wizara hiyo, hata katika Kuzuka kwa Ugonjwa wa Homa kali
ya Mapafu ya Corona.
Mhe, Ummy Mwalimu baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa Tamisemi
amesema Vipaombele vyake katika Wizara hiyo ni kusimamia Halmashauri zote Nchi
kuhakikisha Zinaongeza Mapato ili kusaidia kufanikisha Huduma mbailmbali za
wananchi ikiwemo Afya, elimu na Miundombinu.