Welcome to Mwananyamala Regional Referral Hospital



Mwananyamala Regional Referral Hospital is a public facility serving the population of more than 2.2 million in Dar es Salaam and the surrounding areas, with Kinondoni and Ubungo districts as its definition area. Our Vision is to be a leading Regional Referral Hospital in the provision of Quality Health Services


Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainabu Chaula Akagua Jengo la Mama na Mtoto, Mradi wa Gesi Asilia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.



Katibu Mkuu wa wizara ya Afya maendeleo ya Jamii wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la mama na mtoto pomoja na mradi wa Gasi asilia inayozalishwa hospitalini hapo.


Dkt. Zainabu Chaula ameejionea utekelezwaji wa mradi wa ujenzi wa jingo la Mama Na  Mtoto ambapo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 65.

Baada ya ukaguzi wa jengo la mama na mtoto alitembelea Mradi wa Teknolojia ya uzalishaji wa Gasi asilia kupitia Kondo la Nyuma la uzazi pamoja na mabaki ya chakula ambapo amesema mradi huo utaleta manufaa makubwa nchini pale utakapo endelea kuboreshwa uchakataji wa Taka hizo.


Dkt. Zainabu chaula amepongeza juhudi la uanzishwaji mradi huo  na kusema kuwa utasaidia kuongeza motisha kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa mwananymala.


“uzalishaji wa gasi asilia na fedha zitakazo patikana kutokana na gasi hiyo zitaweza kusaidia uendeshwaji wa huduma za hospitali pamoja na kutoa motisha wa wafanyakazi” alisema Dkt. Zainabu Chaula.


Dkt. Zainabu ameshughudia jinsi gesi hiyo inavyotumika kuchemsha maji kwajili ya matumizi ya wazazi waliojifungua.


Pia. Amezitaka hospitali nyingne nchini kuiga Mfano mzuri wa hospitali hiyo ya Mwananyamala hasa kaitika kuanzisha mradi huo wa uchakataji wa gasi asilia ambao unapunguza uchafuzi wa hali ya hewa pamoja na gharama za matumizi ya umeme.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Daniel Nkungu wakati akimuonyesha miradi huo wa gasi asilia amesema Tangu kuanza uchakataji wa gesi hiyo ni zaidi ya ujazo wa 2237.




Mradi huo wa gasi asilia uliotekelezwa na wizara ya Afya, shirika la umoja wa mataifa la maendeleo UNDP pamoja na Taasisi ya Mazingira duniani.









Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula akitoa maelekezo ya ukamilishaji wa Jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.




Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Tiba (katikati) wakifuatilia Taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya jengo la Mama na Mtoto kutoka kwa watendaji walioko nje ya eneo la ujenzi.





Mganga Mfawidhi akielezea jengo la Mama na Mtoto mbele ya Katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainabu Chaula na Mkurugenzi Ijara ya Tiba Dkt. Grace Magembe.






Viongozi wa idara na vitengo Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ziara ya kukagua juhudi za ukamilishwaji wa jengo la Mama na Mtoto.












Mganga Mfawidhi akiwaongoza ujumbe katika Ziara ya katibu mkuu wa wizara ya Afya kwenye maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa Mwananyamala.

















Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa Mwananyamala Dkt. Daniel Nkungu (Wakwanza kushoto) akitoa maelezo ya hatua za uchakataji wa Gesi Asilia mbele ya Dkt. Zainabu Chaula katibu Mkuu wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto.







Gesi iliyozalishwa kutokana na kondo la nyuma la uzazi na mabaki ya chakula ikitumika kuchemshia maji kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.