Welcome to Mwananyamala Regional Referral Hospital



Mwananyamala Regional Referral Hospital is a public facility serving the population of more than 2.2 million in Dar es Salaam and the surrounding areas, with Kinondoni and Ubungo districts as its definition area. Our Vision is to be a leading Regional Referral Hospital in the provision of Quality Health Services


UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA

 

Mgeni rasmi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitalini hapo tarehe 10 Mei, 2022. Hospitali ya Mwananyamala inatoa bila malipo huduma za afya, upimaji afya na chanjo ya UVIKO kuanzia tarehe 10 Mei hadi siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12 Mei 2022

Afisa Utumishi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Mr. Obeid Ilomo akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhamisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika tarehe 10 Mei, 2022.


Mganga Mfawidhi Dkt .Zavery Benela na Afisa Utumishi Mr. Obeid Ilomo wakifurahia jambo katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 10 Mei, 2022.


Kaimu Muuguzi Kiongozi hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhamisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitalini hapo tarehe 10 Mei, 2022. 

Mgeni rasmi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela akimsikiliza Muuguzi wakati wa ufunguzi wa maadhamisho ya siku ya Wauguzi duniani hospitalini hapo tarehe 10 Mei, 2022.

Baadhi ya Wauguzi mbalimbali wakiburudika kwa pamoja wakati wa ufunguzi wa maadhamisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 10 Mei, 2022.

Muuguzi kutoka kitengo cha TB akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 10 Mei, 2022.

Afisa Ustawi wa Jamii Asia Mkini akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 10 Mei, 2022.




MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI

 

Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Saudan Massawe akizungumza wakati wa maadhamisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani yaliyofanyika hospitalini hapo tarehe 24 Machi, 2022.


Mratibu wa shughuli za Kifua Kikuu, Ukoma na UKIMWI Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Maliwaza Mganga akifanya mahojiano wakati wa maadhamisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani yaliyofanyika hospitalini hapo tarehe 24 Machi, 2022.



Dkt. Prisca Belege akimhudumia mwananchi aliyefika kupatata huduma wakati wa maadhamisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani yaliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 24 Machi, 2022.


Shughuli za utoaji wa elimu ya afya, chanjo ya UVIKO-19 pamoja na upimaji zikiendelea wakati wa maadhamisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani yaliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.



Muelimishaji afya akitoa elimu ya kifua kikuu kwa vijana wa bodaboda mtaani wakati wa maadhamisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani tarehe 24 Machi, 2022 yaliyoandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.


Shughuli za maadhamisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani yakiendelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 24 Machi, 2022.






ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE DKT. GODWIN MOLLEL HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA

 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Dkt. Godwin Mollel akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ziara yake Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 30 Disemba, 2021.

 

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wafanyakazi wakati wa ziara yake Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 30 Disemba, 2021.

 

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Godwin Mollel akiwa katika chumba cha CT-Scan wakati wa ziara yake Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala tarehe 30 Disemba, 2021.

 

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela akitoa taarifa ya hospitali wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Godwin Mollel hospitalini hapo tarehe 30 Disemba, 2021.

 

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Godwin Mollel katika picha ya pamoja Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wakati wa ziara yake hospitalini hapo tarehe 30 Disemba, 2021.

 

 

Muuguzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Musa Wambura akizungumza katika kikao cha wafanyakazi wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Dkt. Godwin Mollel hospitalini hapo tarehe 30 Disemba, 2021.

 

 

Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wakiwa kwenye kikao wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel hospitalini hapo tarehe 30 Disemba, 2021.