Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Akihutubia Baada ya Kuwaapisha Makatibu na
Manaibu katibu wa kuu wa wizara mbalimbali na Wakurgenzi wa Taasisi Mbalimbali Ikulu
Jijini Dar es alaam April 6, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan masema anakusudia Kuunda kamati ya wataalam itakayoangalia Suala la
Ugonjwa wa Corona kitaalam kwa kutumia Tafiti.
Rais Samia Ameyasema Hayo katika Hafla ya kuwaapisha Makatibu
wa mkuu na manaibu katibu wa Mkuu Pamoja na wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali
Leo Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa Kamati hiyo itaishauri
serikali jinsi ya kukabiliana na Ugonjwa Huo.