Katibu Mkuu wa wizara ya Afya maendeleo ya Jamii wazee na Watoto
Dkt. Zainabu Chaula ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na
kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la mama na mtoto pomoja na
mradi wa Gasi asilia inayozalishwa hospitalini hapo.
Dkt. Zainabu Chaula ameejionea utekelezwaji wa mradi wa ujenzi
wa jingo la Mama Na Mtoto ambapo mpaka
sasa umekamilika kwa asilimia 65.
Baada ya ukaguzi wa jengo la mama na mtoto alitembelea Mradi
wa Teknolojia ya uzalishaji wa Gasi asilia kupitia Kondo la Nyuma la uzazi
pamoja na mabaki ya chakula ambapo amesema mradi huo utaleta manufaa makubwa
nchini pale utakapo endelea kuboreshwa uchakataji wa Taka hizo.
Dkt. Zainabu chaula amepongeza juhudi la uanzishwaji mradi huo
na kusema kuwa utasaidia kuongeza
motisha kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa mwananymala.
“uzalishaji wa gasi asilia na fedha zitakazo patikana kutokana
na gasi hiyo zitaweza kusaidia uendeshwaji wa huduma za hospitali pamoja na kutoa
motisha wa wafanyakazi” alisema Dkt. Zainabu Chaula.
Dkt. Zainabu ameshughudia jinsi gesi hiyo inavyotumika
kuchemsha maji kwajili ya matumizi ya wazazi waliojifungua.
Pia. Amezitaka hospitali nyingne nchini kuiga Mfano mzuri wa
hospitali hiyo ya Mwananyamala hasa kaitika kuanzisha mradi huo wa uchakataji
wa gasi asilia ambao unapunguza uchafuzi wa hali ya hewa pamoja na gharama za
matumizi ya umeme.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala
Dkt. Daniel Nkungu wakati akimuonyesha miradi huo wa gasi asilia amesema Tangu kuanza
uchakataji wa gesi hiyo ni zaidi ya ujazo wa 2237.
Mradi huo wa gasi asilia uliotekelezwa na wizara ya Afya,
shirika la umoja wa mataifa la maendeleo UNDP pamoja na Taasisi ya Mazingira
duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Zainabu Chaula akitoa maelekezo ya ukamilishaji wa Jengo la Mama na Mtoto
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Tiba (katikati)
wakifuatilia Taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya jengo la Mama na Mtoto kutoka
kwa watendaji walioko nje ya eneo la ujenzi.
Mganga Mfawidhi akielezea jengo la Mama na Mtoto mbele ya Katibu mkuu Wizara
ya Afya Dkt. Zainabu Chaula na Mkurugenzi Ijara ya Tiba Dkt. Grace Magembe.
Viongozi wa idara na vitengo Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala wakimsikiliza
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa
ziara ya kukagua juhudi za ukamilishwaji wa jengo la Mama na Mtoto.
Mganga Mfawidhi akiwaongoza ujumbe katika Ziara ya katibu mkuu wa wizara
ya Afya kwenye maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa Mwananyamala.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Daniel Nkungu (Wakwanza kushoto) akitoa maelezo ya hatua za uchakataji wa Gesi Asilia mbele ya Dkt. Zainabu Chaula katibu Mkuu wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto.
Gesi iliyozalishwa kutokana na kondo la nyuma la uzazi na mabaki ya chakula ikitumika kuchemshia maji kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.