Welcome to Mwananyamala Regional Referral Hospital



Mwananyamala Regional Referral Hospital is a public facility serving the population of more than 2.2 million in Dar es Salaam and the surrounding areas, with Kinondoni and Ubungo districts as its definition area. Our Vision is to be a leading Regional Referral Hospital in the provision of Quality Health Services


UMMY AAPISHWA KUWA WAZIRI WA TAMISEMI BAADA YA KUTEULIWA NA RAIS SAMIA SULUHU

Mhe. Ummy Mwalimu akila kiapo Baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa TAMISEMI, 1 April 2021 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

DODOMA. Aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na maziringa Mhe, Ummy Mwalimu amekula kiapo cha kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Mhe. Ummy ameapishwa katika Hafla iliyofanyika Tarehe 2 April 2021 Ikulu ya Chamwino Jijini Dododma ya kuwaapisha Mawaziri wa wizara Mbalimbali walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Awali Wizara hiyo ya TAMISEMI ilikuwa ikisimamiwa na Mhe, Suleiman Jaffo ambaye aliteuliwa na Hayati Magufuli akiwa Raisi na kudumu kwenye Nafasi hiyo kwa kipindi cha Maika mitano ya awamu ya Tano.

 

Kabla ya Mhe. Ummy Mwalimu kushika Nyazfa hizo Mbili Alikuwa Waziri wa Afya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Kipindi cha Miaka Mitano ya Awamu ya Tano Baada ya kuteuliwa na Aliyekuwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Katika Kipindi alichokuwa waziri wa Afya Mhe Ummy alisimamia Kikamilifu Wizara hiyo, hata katika Kuzuka kwa Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu ya Corona.

 

Mhe, Ummy Mwalimu baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa Tamisemi amesema Vipaombele vyake katika Wizara hiyo ni kusimamia Halmashauri zote Nchi kuhakikisha Zinaongeza Mapato ili kusaidia kufanikisha Huduma mbailmbali za wananchi ikiwemo Afya, elimu na Miundombinu.